March 20, Miss Singida 2014/15, Doris
Mollel alizindua Foundation aliyoipa jina la Doris Mollel Foundation
ambayo itakayohusika kukusanya mapato yatakayowasaidia watoto
wanaozaliwa kabla ya kufikisha miezi 9 ‘Watoto njiti’.
Akizungumza kwenye mkutano huo na waandishi wa habari mwenyekiti wa mfuko huo, Doris Mollel
amesema lengo la mfuko huo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia jamii
katika upande wa watoto njiti ambapo takwimu zilizopo zinaeleza idadi ni
ndogo kutokana na jamii nyingine hazina utamaduni wa kwenda
kujifungulia katika vituo vya afya hivyo elimu inahitajika kufanya jamii
hizi zifike katika vituo vya afya na kuwezeshwa kwa vituo hivyo kuwa na
vifaa ili kupunguza vifo vya watoto njiti 9000.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga
na mimi kwa kubonyeza
No comments:
Post a Comment