Rais Barack Obama wa Marekani alikutana na vijana mbalimbali kutoka bara la Afrika ikiwa
ni mpango wa serikali yake kila mwaka toka mwaka 2014 kukutana na
vijana hao wanaohusika na kuivusha jamii kwenye ishu mbalimbali ikiwemo
biashara na siasa.
Mwanaharakati
wa haki za binadamu Mtanzania Mwanasheria Geline Fuko kutokea kwa
Hellen Kijobisimba kwenye kituo cha sheria na haki na bianadamu ni
miongoni mwa vijana takribani 40 kutoka Tanzania ambao walishinda nafasi
za kuja Marekani kwenye huo mpango wa Obama.
Nafasi
hiyo ameipata baada ya kushiriki katika kutengeneza kanzidata ya katiba
ambayo inatoa nafasi kwa watanzania kusoma mambo mbalimbali ya katiba,
Usiku wa August 5 2016 Geline Fuko amerejea Tanzania na ametoa wito wake
kwa serikali ya Tanzania kuhusu mchakato wa katiba mpya, Fuko amesema……
>>>’kilio
cha watanzania kuhusiana na katiba bado kipo na mchakato tulishauanza
ni vyema tukauamaliza katika namna ambayo kila mwananchi atapata nafasi
ya kuridhika na namna mchakato utakavyokwenda, wito wangu kwa serikali
mchakato wa katiba tunaomba muurudishe na muwakabidhi wanachi jukumu la
kumalizia mchakato huu kwa namna wenyewe watakavyoona unafaa’
No comments:
Post a Comment