Msafara
 wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa umekwama 
kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi  baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba
 unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea 
mikoa hiyo.
Lowassa
 ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake  mkoani 
Mbeya tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo 
yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake  mkoani  Songwe wakati leo 
asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.
Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya  Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.
Katibu
 wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, 
Frank Mwaisumbe  alisema  kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa
 1.00 jioni akiwa Tunduma  wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.
Kamanda
 wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa  kwa njia ya simu 
alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara 
kwa sababu  mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.

 
No comments:
Post a Comment