Mashuhuda 
 wa ajali iliyosababisha kifo cha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake 
Tanzania (UWT) Mkoa wa Dodoma, Salome Kiwaya wamesema alikufa kutokana 
na kushindwa kupewa msaada kwa haraka.
Walisema
 baada ya ajali walisikia sauti za watu wakilia kuomba msaada lakini 
ilichukua muda wa sasa tatu ndipo walipopata msaada wa kuokolewa 
kutokana na ukosefu wa vifaa vya uokoaji.
Juzi
 katika eneo la Emmaus mkoani hapa ilitokea ajali ya gari la Toyota Noah
 na lori ambayo ilichukua maisha ya Mwenyekiti huyo na watu wengine 
watatu kujeruhiwa. 
Mmoja wa mashuhuda hao Amri Juma alisema alisikia sauti za wanawake wakiomba msaada ili waweze kuokolewa.
“Ni
 jambo la kusikitisha kuona zaidi ya saa tatu hakuna vifaa vya uokoaji 
vilivyokuwa vimefika kwa ajili ya uokoaji, ajali ilitokea saa nane 
mchana lakini mpaka saa 11 jioni ndio watu wanakuja kutolewa.
‘’‘Breakdown
 moja ilipofika ilishindwa kunyanyua lori, ilipofika ya pili ilishindwa,
 hali inayoonesha kuna uhaba wa vifaa hivyo mamlaka husika zijipange 
kuwa na vifaa vya uokoaji."
 Juma
 alisema Dodoma imeanza kuandaliwa kuwa makao makuu ya nchi hivyo wakati
 umefika wa kuanza kujengewa uwezo wa kuwa na vifaa vya kisasa vya 
uokoaji. 
Katibu wa UWT Mkoa wa Dodoma, Kaundime Kasase, akizungumzia kifo hicho alisema;
“imeniuma
 sana na bado inaniuma, sina hata la kusema kwani nimefanya naye kazi 
kwa ukaribu, alikuwa mtu anayependa viongozi wake wote."
Mtoto aliyekuwa ndani ya gari hilo, Dearest Mabuba (8) alisema; “Tulikuwa
 tumetoka kwenye birthday (siku ya kuzaliwa) yangu ndipo gari likapata 
ajali, mama yangu Annastazia Amandus ambaye alikuwa akiendesha gari hilo
 akaumia kichwani na dada akachanika kwenye kiwiko,” alisema.
Meya wa Manispaa ya Dodoma, Jaffari Mwanyemba alisema wamempoteza mtu muhimu.
“Alikuwa akijichanganya kila mahali, tumepoteza mtu muhimu tuige mazuri yake”. 
Mbunge wa Viti Maalumu na Mwenyekiti mstaafu wa UWT Mkoa wa Dodoma, Fatma Tawfiq alisema;
“Mwenyezi Mungu ndiye alikuwa akifahamu siri hii. “Ni jambo la kushtukiza sana tumuombee Mungu amuweke mahali pema peponi,” alisema.
Hata
 hivyo kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa 
Dodoma, Marson Mwakyoma alisema walifika eneo la tukio dakika 10 baada 
ya ajali hiyo kutokea.
“Si
 lazima askari avae sare tulifika mapema na vikosi vingine vya uokoaji 
vilikuja kwa wakati, nadhani kitu muhimu kinachotakiwa kufanyika ni 
kuimarisha vifaa vya uokoaji,” alisema.

 
No comments:
Post a Comment