Tuzo za MTV Europe Music 2016 zilifanyika weekend iliyopita ambapo Mnigeria staa wa single ya Baba Nla Wizkid alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo ya BEST AFRICAN ACT tofauti na ilivyokuwa ikionesha kwenye kura za mtandaoni kuwa Alikiba ndiye mshindi.
Mjadalia mkali ulianza mitandaoni kuhusu mshindi halali wa tuzo ya MTV EMA kwenye category ya BEST AFRICAN ACT, ambapo uliwafikia waandaji wa tuzo hizo.
Leo
November 10 2016 MTV Base East kupitia akaunti yao ya twitter
wametangaza rasmi kuwa tuzo hiyo aliyestahili kuipata ni mtanzania Alikiba na wamempongeza kwa tuzo hiyo .
No comments:
Post a Comment