LOS ANGELES, Marekani
MUME wa Khloe Karda-shian, Lamar Odom, ameruhusiwa kutoka hospitalini kwa ajili ya kupata uangalizi mzuri nyumbani lakini habari ni kwamba, Khloe amekataa kumpokea Lamar na sasa watu wake wa karibu wanahangaika pa kumhifadhi staa huyo wa zamani wa mpira wa kikapu.
Lamar Odom.
Tangu Oktoba 13, mwaka huu, Lamar alikuwa amelazwa hospitalini
kutokana na kuzidisha matumizi ya madawa ya kulevya, lakini licha ya
ndoa yao kuwa kwenye mtafaruku, Khloe alikuwa bega kwa bega kumuuguza
mumewe huyo mpaka amepata nafuu lakini ghafla mambo sasa yamebadilika
baada ya Lamar kuruhusiwa kutoka hospitali.“Baada ya hospitali, Lamar sasa anahitaji uangalizi mzuri, lakini Khloe ametuchanganya baada ya kukataa kumpokea Lamar nyumbani kwake.
Anaonekana hatanii katika hili, maana haonyeshi dalili yoyote ya ushirikiano wa kumpa huduma mumewe baada ya kutoka hospitali,” alisema mtu wa karibu na familia hiyo.
aarifa nyingine inasema hata watoto wa Lamar waliokuwa wanakwenda hospitali kumjulia hali baba yao, nao hawana mpango wa kumpokea mzee wao kwa sasa.
No comments:
Post a Comment