Monday, December 7, 2015

MBINU 5 ZA KUJIFUNZA MAPENZI ILI USIACHIKE, USISALITIWE!


Nilishawahi kusema huko nyuma kwamba, mapenzi yanachukuwa sehemu kubwa sana ya maisha yetu ya kila siku.

Tunafanya kazi usiku na mchana lakini pesa tunazopata tunazitumia kwenye kufurahia maisha na wapenzi wetu.Ndiyo maana ukiwa hauko sawa kimapenzi, namaanisha ukiwa huna mpenzi wakati unahitaji kuwa naye au unaye lakini anakukorofisha, hata mambo mengine huwezi kuyafanya kwa ufasaha.
 

Lakini yule ambaye maisha yake ya kimapenzi yako sawa, anapata anachokitaka kutoka kwa mpenzi wake, utagundua anafanya kazi kwa ufanisi mkubwa na furaha haikauki.

Wakati ukweli ukiwa hivyo, wapo ambao wanaachika kila siku kwa sababu ya kushindwa kujua namna ya kuwashika wapenzi wao. Kuna ambao kusalitiwa kumekuwa ni sehemu ya maisha yao kwa sababu hawajui yapi wayafanye ili wapenzi wao wasifikirie kutoka nje ya uhusiano wao.

Kimsingi nimegundua wengi hatuna elimu ya kutosha juu ya mapenzi. Unakuta mtu kaanzisha uhusiano na mtu ambaye yuko mbali lakini hajui wanawezaje kulidumisha penzi lao. 

Mmeoana wote mnafanya kazi na ni wanandoa, mnawezaje kuishi katika msingi sahihi? Hayo yote utayajua endapo tu utajua sehemu sahihi ya kuweza kujifunza na kuwa na ufahamu kuhusu mambo hayo.

Huenda wewe tangu umezaliwa hujawahi kujihusisha kimapenzi, leo umeingia kwenye uhusiano na hujui chochote, kama huna elimu ya mapenzi hata kama umzuri vipi, utaachika tu kama siyo kusalitiwa kila siku.

Ndiyo maana leo nimeleta mada hii ili kama ulikuwa hujui, uanze leo kujiimarisha kwenye masuala ya mahaba. Kumbuka hapa nazungumzia mapenzi ya kiutu uzima, yale ambayo huwezi kufundishwa shuleni. 
Mtandaoni
Mitandao imekuwa ni msaada sana katika ulimwengu wa sasa. Hakuna ambalo utalihitaji usilipate kwenye mtandao. Kwa maana hiyo basi, kama kuna jambo unataka kulijua kuhusu mapenzi, kuwa rafiki wa mitandao husika.

Kwa mfano unataka kujua jinsi unavyoweza kumfurahisha mpenzi wako mkiwa faragha. Ukiuliza mtandao, utakuletea.Licha ya kwamba lugha unayotumika ni ya Kiingereza, naamini wengi wetu tunajua hata kama ni cha kubangaiza. Ila zipo baadhi ya mada ukiandika kwa Kiswahili pia unaweza kuzipata.

Majarida maalum
Yapo majarida yanayozungumzia mapenzi kwa undani wake ambayo yanauzwa sehemu maalum kwa jili ya watu wazima tu. Kama kweli wewe ni mtu mwenye uhitaji wa majarida hayo, ukiulizia utayapata kwani huwezi kuyakuta yanauzwa kiholela.

Wakati mwingine yanauzwa bei kubwa lakini elimu utakayoipata ni kubwa na huwezi hata kujutia fedha uliyotoa. Kwa mfano unanunua jarida la shilingi 50,000 na ndani yake ukapata mada juu ya kuishi kwa furaha na mpenzi wako, namna na kuidumisha ndoa yako, jinsi ya kumpagawisha mpenzi wako muwapo faragha na kadhalika. Huoni itakuwa ni pesa ndogo ukilinganisha na gharama ulizotumia kwenye harusi yenu?

Ongea na wataalam
Kuna wataalam wa mambo ya mapenzi ambao wanaweza kukusaidia. Kwa mfano mimi nimekuwa nikitumia muda wangu mwingi kushauri wasomaji wangu juu ya mambo yanayowakosesha furaha katika maisha yao ya kimapenzi.

Siyo mimi tu, wapo wengi wakiwemo baadhi ya akina mama ambao wamekuwa wakitumika sana kwenye kuwafunda wasichana kabla ya kuingia kwenye ndoa.Kikubwa ni kujua watu sahihi wa kuwauliza mambo sahihi kuhusiana na mapenzi. Nilichogundua mimi ni baadhi ya watu kuwa na aibu. Hivi unaonaje aibu huku unataka kujua mambo nyeti ambayo unajua kutokuyafahamu kunaweza kuihatarisha ndoa yako?

Angalia vipindi vya kikubwa
Kwa watu wenye uchu na elimu hasa hii nyeti, inabidi wakati mwingine wakubali kuamka usiku na kuangalia vipindi ambavyo vinazungumzia mapenzi kwa watu wazima.Mara nyingi vipindi hivi huwezi kuviona mchana, wanaovirusha husubiri muda ambao watoto wamelala. Ukiwa ni mpenzi wa kuvifuatilia vipindi hivi, ni lazima utakuwa bora kwenye uhusiano wako.


Nunua CD
Huenda hata wewe una CD zako ambazo mara nyingi unaziangalia usiku kabisa, ukiwa peke yako au na mwenza wako. Hilo ni jambo zuri hasa linapokuja suala la kujiweka fiti kimapenzi.
Katika hili naomba niseme tu kwamba, kuna ambao wanazitumia CD hizi kujiharibu. Wanazinunua ili kujifunza mambo kadhaa lakini mwisho wake wananogewa na kujikuta wakimaliza haja zao kwa kuziangalia.

Niwaonye tu kwamba, ukizoea sana kuziangalia picha hizo ukiwa peke yako kisha ukamaliza shida zako, unaweza kujikuta si mtu unayependa kuwa na mpenzi tena. Wapo ambao leo hii hawataki kusikia kitu mpenzi, kisa wakiangalia CD hizo humaliza haja zao! Ni sawa unaweza kumaliza haja zako lakini madhara yake ni makubwa. Ndiyo maana nasema kwamba, tumia CD hizo kujipatia ujuzi lakini si kumalizia haja zako.
Ni hayo tu ila kama unataka kujifunza zaidi kupitia mimi, usisite kunitafuta. Kumbuka ujanja na ubunifu wako ndivyo vinaweza kudumisha ndoa yako lakini ukiwa unaendesha maisha yako kibubusa, kaa mkao wa kusalitiwa kama siyo kuachwa!

No comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system