Wednesday, January 20, 2016

Hii hapa ripoti ya Daktari feki kutoka Hospitali ya Sekouture Mwanza.


Ripoti iliyonifikia kutokea Mwanza ni hii ya kukamatwa kwa Daktari feki kwenye hospitali ya Mkoa ya Sekouture Mwanza, mtuhumiwa anajulikana kwa jina la David Igwesa amekamatwa baada ya kuomba pesa kwa mgonjwa kiasi cha shilingi 500,000.
Baada ya mgonjwa kuona muda unapita bila kupatiwa matibabu akaamua kwenda kwa Kaimu Mganga mfawidhi Dk Bahati Msaki kumueleza ndipo wakaanza kumtafuta na kumakamata…ninazo sentensi za Mganga mfawidhi akieleza kutana nazo; – Bahati Msaki Kaimu Mgaga Mfawidhi
Alikuja mgonjwa anaitwa Dotto alitakiwa kufanyiwa upasuaji akawa analalamika alikutana Daktari mapokezi akamwambiwa ampe laki tano ili amfanyie upasuaji nikamwambia twende ili niweze kumtambua nilimuita ofisini;Dk Bahati Msaki
Image00002
Daktari feki David Igwesa mbele ya wanahabari
Sikuweza kumfahamu sio Daktari muajiriwa na wala sio wale Madaktari ambao wapo katika mafunzo katika kumuuliza akashindwa kujieleza yeye ni mtu wa aina gani tukagundua huyu ni wale matapeli wanaotapeli wagonjwa wanakuja wanajifanya madaktari mwisho wa siku wanawachukulia wagonjwa hela bila kuwapatia risiti; – Dk Bahati Msaki Kaimu Mgaga Mfawidhi Sekouture.
Image00003

No comments:

Post a Comment

Disqus Shortname

Comments system