Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia
salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais
Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kufuatia kifo cha
Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) Bi. Asha Bakari
Makame kilichotokea jana tarehe 19 Januari, 2016 huko Dubai.
Bi.
Asha Bakari Makame ambaye kwa nyakati tofauti amewahi kuwa Waziri
katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mjumbe wa Baraza la
Wawakilishi, amekutwa na mauti akiwa safarini kurejea Zanzibar akitokea
nchini India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu.
Katika
Salamu zake za rambirambi Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Asha
Bakari Makame kuwa alikuwa Kiongozi Hodari, Mchapakazi na aliyeipigania
nchi yake hususani Muungano wa Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar.
Amemuomba
Mwenyekiti wa CCM Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kumfikishia salamu za pole
kwa Viongozi wa Chama na Serikali ya Zanzibar, wanaCCM, Ndugu na jamaa
wote wa Marehemu walioguswa na msiba huu mkubwa.
"Nimesikitishwa
sana na kifo cha Bi. Asha Bakari Makame na namuombea kwa Mwenyezi Mungu
aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina" Alisema Dkt. Magufuli.
Gerson Msigwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU.
Dar es salaam.
20 Januari, 2016.
Mpekuzi blog
No comments:
Post a Comment