
Chuo Kikuu cha Mt. Joseph
kimechukua vichwa vya habari hivi karibuni baada ya kutokea kwa migomo
kwenye vyuo vishiriki vya chuo hicho na baadhi kufutiwa vibali
vilivyoanzisha vyuo vikuu viwili vishiriki vya Mt Joseph ambavyo
ni chuo kikuu kishiriki cha sayansi ya kilimo na Teknolojia ‘SJUCAST’
na chuo kikuu kishiriki cha teknolojia ya Habari Mawasiliano ‘SJUIT’.
Chuo cha Mt Joseph
nao waligoma kuanzia mwanzoni mwa juma hili wakiwa na madai mbalimnbali
ikiwemo kufundishwa mtaala ambao haupo nchini pamoja na wakufunzi wasio
na sifa.
Leo March 9 Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako amefika chuoni hapo na kutoa maelezo ikiwa ni juhudi za kutatua mzozo huo na ameyazungumza haya kwa wanafunzi…
>>>’baada
ya kuona changamoto nyingi kuwa ni za kiutawala, kwa hiyo mmalizie
mitihani yenu, baada ya mitihani ni wiki mbili, kwa hiyo chuo kitakuwa
kimefungwa, muda huo Chuo kirekebishe dosari ndogondogo hizi za kwenye
maabara, vitu ambavyo havijafungwa na vimekwisha kufika vifungwe na
kikubwa zaidi ni suala la kiutawala kwa wale ambao hawana sifa Utawala
urekebishe‘:-Joyce Ndalichako
Pia Waziri Ndalichako amegusia madai ya ada kubwa chuoni hapo na ameyazungumza haya
>>> ‘suala
la ada ni suala ambalo linatakiwa liangaliwe kwa ujumla wake kwa vyuo
vyote kwa sababu mwanafunzi anapojiunga na chuo anajua ada ni kiasi
kadhaa, kwa hiyo kwa kusema kwamba itapungua hilo ni suala la
makubaliano, na kwa kuzingatia kwamba TCU inaangalia namna ya kuweka ada
elekezi kwa vyuo vyote kwa hiyo sasa hivi wanafunzi watatakiwa kulipa
ada kama makubaliano yalivyo wakati makubaliano yale yanaendelea’:– Joyce Ndalichako
No comments:
Post a Comment