Mpekuzi blog
Waziri mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye jana alitangaza rasmi kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) na akakabidhiwa kadi na Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe.
Sumaye
ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa CCM na kudai kuwa
anaunga mkono mageuzi yanayofanywa na vyama vinavyounda katiba ya
wananchi (UKAWA) bila kuweka wazi kuwa yuko kwenye chama kipi kati
ya hivyo amesema sasa ameamua kujiunga na CHADEMA.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa jimbo la Arusha kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya Baraa, Sumaye alisema anataka kuungana na wanamageuzi wenzake katika kuendeleza harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado zinaendelea.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe alisema
chadema na vyama washirika wa UKAWA bado viko imara na vimeendelea
kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi azma yao ya kuleta
ukombozi nchini iko pale pale.
No comments:
Post a Comment