KATIBU
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amemjibu aliyekuwa mgombea urais wa
Chadema, Edward Lowassa, aliyedai kuwa kazi nzuri anazofanya Rais John
Magufuli, ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa).
Akizungumza
na wananchi katika mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa
Arusha, Philemon Mollel (Monaban), uliofanyika katika kata ya Daraja
Mbili jana, Kinana alisema sera ya kupambana na ufisadi ilizungumzwa
katika kampeni na Dk Magufuli peke yake na si Lowassa wala kiongozi
yeyote wa Ukawa.
Kinana
alisema anamshangaa kiongozi huyo kwa kuwa mbali na kushindwa
kuzungumza wakati wa kampeni za urais, pia hakuwa na hotuba yoyote
ambayo ingeweza kukaririwa na Dk Magufuli.
Alisema
Lowassa hakuweza kuzungumzia masuala yoyote ya kupambana na ufisadi kwa
kuwa yeye ni mtuhumiwa na vyama vina vyounda umoja huo ndiyo
vimekumbatia ufisadi kwa sasa.
Kwa
mujibu wa Kinana, Lowassa alinadi sana mabadiliko kama angeweza kuingia
madarakani, lakini hakufafanua ni mabadiliko yapi ambayo angeweza
kuyaleta, wakati anatoka katika mfumo ule ule aliokulia kwa zaidi ya
miaka 40 akiwa ndani ya CCM na Serikali yake.
“Jamani
Lowassa alisema mabadiliko lakini hao wanaotaka mabadiliko wana umri wa
ujana sawa na jua linalochomoza la saa mbili asubuhi, wakati yeye
anayedai kuleta mabadiliko ana umri wa uzee sawa na jua linalozama la
saa 12.30 jioni, si vichekesho hivyo?” Alihoji Kinana.
Alisema
kutokana na ukweli huo, ndiyo maana Watanzania walipima na kuamua kumpa
ushindi wa kishindo Dk Magufuli, kutokana na uadilifu wake pamoja na
uwezo wake wa kuchapa kazi na kuamua kumnyima Lowassa na ndiyo maana kwa
sasa anajifariji kwa kusema sera zinazotekelezwa ni za Ukawa.
Akizungumzia
kazi alizoanza kuzifanya Rais Magufuli, Kinana alisema zimewakuna
Watanzania wengi na kusema kuwa hiyo ndiyo kazi aliyoahidi kwao kuifanya
na kwamba anaamini ataifanya kwa dhati katika kuwapigania wananchi
wanyonge.
Mfumo wa CCM
Akizungumzia madai kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya Serikali, kwa kuwa hilo ni suala la mfumo, Kinana alipinga na kusema si kweli.
Akizungumzia madai kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya Serikali, kwa kuwa hilo ni suala la mfumo, Kinana alipinga na kusema si kweli.
Akifafanua
alisema mfumo unaweza kubadilishwa hata na mtu mmoja kama anavyofanya
Dk Magufuli, Makamu wake, Mama Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu,
Kassim Majaliwa.
Alisema
moja ya mambo aliyoyaondoa Magufuli katika mfumo huo, ni pamoja na
kufuta safari za nje kwa viongozi akiwemo yeye binafsi, kuondoa semina,
warsha, makongamano, sherehe na maadhimisho mbalimbali pamoja na posho
mbalimbali na kuagiza fedha hizo kwenda katika mahitaji mengine ikiwemo
hospitalini.
Akizungumzia
uchaguzi wa ubunge unaotarajiwa kufanyika Desemba 13 mwaka huu, Kinana
aliwataka wananchi wa Jimbo la Arusha Mjini, kuachana na ushabiki wa
vyama na badala yake wachague kiongozi kutokana na sifa zake na
kuangalia maslahi yao na siyo ya chama wala kiongozi husika.
Alisema
kwa sasa wananchi wa jimbo hilo wanapaswa kuangalia maslahi yao katika
kumchagua mbunge, yakiwemo maslahi ya shule, afya, miundombinu, amani
pamoja na mambo mengine mengi, badala ya kubaki kuimbiwa kuwa
wanafundishwa kuiwajibisha Serikali huku wakibaki katika lindi la
umasikini, ukosefu wa amani na maandamano kila kukicha.
No comments:
Post a Comment