Shirikisho la soka barani Afrika
CAF lenye makao makuu yake
Cairo Misri, leo February 3 2017 kupitia kwa shirikisho la soka
Tanzania TFF limeipitisha timu ya taifa ya
Tanzania ya vijana chini ya umri wa miaka 17 (
Serengeti Boys) kupata nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya Afrika kwa vijana
(AFCON-U17).
CAF wametoa taarifa hizo baada ya
Tanzania kushinda rufaa yao waliyoikata dhidi ya timu ya
Congo Brazzaville ambao walichezesha mchezaji aliyezidi umri wakati wa mchezo dhidi ya
Serengeti Boys, hivyo
Serengeti Boys wanapewa nafasi hiyo baada ya
Congo kushindwa kumpeleka mchezaji wao aliyedaiwa kuzidi umri kufanyiwa uhakiki wa umri wake.

Langa Lesse Bercy anayedaiwa kuzidi umri pichani kulia
Kama utakuwa unakumbuka vizuri shirikisho la soka
Tanzania TFF lilikata rufaa kwa
CAF kupinga
Congo kumchezesha mchezaji
Langa Lesse Bercy aliyedaiwa kuvuka umri wa miaka 17, hivyo alicheza mchezo dhidi ya
Serengeti Boys kimakosa
.

Tweet ya Waziri wa michezo Nape Nnauye
No comments:
Post a Comment