Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo, amewasimamisha kazi watumshi watatu
wa Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, kutokana na kuruhusu ujenzi wa
nyumba juu la bomba la mradi wa maji na kuamuru ivunjwe mara moja.
Mulongo
alitoa maagizo hayo jana baada ya kuitisha kikao cha dharura cha wakuu
wa idara ya halmashauri hiyo kutaka kufahamu chanzo cha ujenzi wa nyumba
hiyo baada ya kupata taarifa ya mradi wa maji ulioanza mwaka 2005 na
kugharimu Sh. bilioni 20.
“Kuanzia
sasa natoa agizo la kuwasimamisha kazi watendaji watatu wa halmashauri
ambao ni Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira,
Nestory Kabete, Kaimu Afisa Ardhi, Richard Pungu, pamoja na Mkuu wa
Kitengo cha Mipango Miji, Wilson James, baada ya kushindwa kutekeleza
kazi walizopewa na serikali,” alisema Mulongo.
Alisema
watumishi hao kwa pamoja walipuuzia na kukaidi amri ya serikali
waliyoitoa ya siku 21 ya kubomoa nyumba iliyojengwa juu ya mradi wa maji
inayomilikiwa na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo,
Pamphil Masashua, tangu Juni mwaka huu, hali iliyosababisha mradi huo wa
maji kusuasua.
Alisema
wataalam wa maji na ardhi wanatakiwa kwenda ofisi za mkoa huo kuanzia
jana ili wafanyie uchunguzi wa kina na iwapo watabaini nyumba hiyo ni
mali ya Masashua na imejengwa juu ya miundombinu ya maji lazima
ibomolewe haraka.
“Na
yeyote aliyeshiriki katika kutoa kibali cha ujenzi na ramani ambavyo
havikuwa sahihi, lazima watafikishwa mbele ya mahakama,” alisema.
Aidha,
Mulongo alimtaka katibu tawala wa mkoa huo, kuwahamisha watumishi wa
idara ya ardhi pamoja na wanasheria wa halmashauri hiyo kwa kufanya kazi
kwa mazoea na kusababisha wananchi kubuni mbinu mbadala za kuhujumu
serikali.
Katika
hatua nyingine, Mulongo alimuagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Sengerema,
Julius Chaliya, na Katibu Tawala, Ndaro Kulijila, kuhakikisha wanawalipa
walimu 234 pesa zao za mishahara ikiwa ni pamoja na barua za
kuwaidhinisha kupanda vyeo kuanzia 2014/15 haraka iwezekanavyo.
No comments:
Post a Comment